Paul Makonda Atowa Msaada Wa Million 80 Kwa Matibabu Ya Uyu Kijana Soma Zaidi Hapa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amejitolea kumsaidia kijana Ahmed Albaity anayesumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo lililompelekea kulala kitandani kwa takribani miaka 10. Kijana huyo anatakiwa kwenda kutibiwa nchini China kwa muda wa wiki tatu akiambatana na wasaidizi wawili ambapo gharama za matibabu zinazohitajika ni zaidi ya dola 40,000 za marekani ambapo sindano moja aliyoandikiwa inagharimu kiasi cha dolla 27,000. RC Makonda amesema atafanya jitihada zote kuhakikisha Ahmed anapatiwa Matibiwa ili aweze kupona na kutimiza ndoto zake akiwa na Afya Njema. Mapema leo RC Makonda ametembelewa ofisini kwake na Balozi mpya wa China Nchini Tanzania Bi. Wang Ke ambae amekuja kujitambulisha kwa Mkuu wa Mkoa ambapo katika mazungumzo RC Makonda amemgusia balozi huyo suala la matibabu ya AHMED ALBAITY ambapo Balozi WANG KE alieambatana pia na Daktari Bingwa wa China aliebaki Nchini kwaajili ya Shughuli ya Serikali ya China ambapo wamemtazama na kupitia Ripoti ambapo wameah...