Uwezi Amini Alichosema MAMA Kanumba Kuhusu Kwenda Jela Kumsalimia LULU Angalia Hapa
MAMA wa aliyekuwa muigizaji nguli wa filamu nchini, Steven Kanumba, Flora Mtegoa, amesema kuwa ataongea na Mungu wake kama ataweza kwenda kumuona muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, ambaye yuko gerezani kwa sasa kufuatia hukumu ya kifungo cha miaka miwili alichohukumiwa na Mahakama Kuu jijini Dar, baada ya kukutwa na hatia ya kumuua Kanumba bila kukusudia.
Mama Kanumba aliyasema hayo alipokuwa katika uzinduzi wa Filamu ya Zero Player, aliyocheza mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto, ambayo ilizinduliwa jana Ijumaa katika Ukumbi wa Suncrest Sunplex uliopo Quality Center jijini Dar.
Comments
Post a Comment