Mwalimu Atupwa Jela Mwaka 1 kwa Kosa la Kumtongoza na Kumtumia Picha za utupu Mwanafunzi Wake
Mwalimu wa somo la Mapishi katika shule ya Sekondari ya St. Charles High School mjini Maryland nchini Marekani amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kumtongoza na kumtumia picha za utupu mwanafunzi wake wa kiume mwenye umri wa miaka 17.
Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwenye mtandao wa kituo cha runinga cha Fox 5 DC Mwalimu huyo aliyetambulika kwa jina la LaToya Nicole Parker (40) imeelezwa kuwa alikuwa anamtuma mwanafunzi huyo kwenye supermarket kipindi cha mapumziko na kwenda nae nyumbani kwake.
Kisa hicho ambacho kiliripotiwa na wazazi wa mwanafunzi huyo mwezi machi mwaka huu, 2017 kwenye kituo cha polisi kabla ya kupelekwa mahakamani ambapo mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo jumatatu ya wiki iliyopita.
Upelelezi uliofanywa na polisi pamoja na ushahidi uliotolewa mahakamani unaonesha kuwa mwalimu huyo alianza kumtongoza mwanafunzi huyo tangu mwezi April mwaka huu , 2017 kwa kumuandikia barua za mahaba, kumtumia picha zake za utupu na kumuahidi pesa mwanafunzi huyo kama angelikubali.
Kwa upande mwingine mwalimu mkuu wa shule ya St. Charles High School Principal, Richard Conley amesema mwalimu huyo alikuwa anafundisha somo la Mapishi shuleni hapo na alikuwa hajaajiriwa rasmi shuleni hapo bali alikuwa anafanya kazi kwa muda (Temporary) tangu mwezi Machi mwaka huu 2017.
“Baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wazazi wake mapema tulimsimamisha kazi Ms. Parker kwani tayari walikuwa wameshatoa taarifa polisi ili kupisha uchunguzi.“amesema Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Richard Conley.
Polisi mjini Maryland wamesema walikuta picha 5o za utupu za mwalimu huyo na jumbe 303 zilizotumwa kwenye simu ya mwanafunzi huyo nyingi zikiwa za mahaba.
Mahakama mjini Maryland inayoshughulikia kesi za watoto imetoa hukumu kwa mwalimu huyo kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini ya dola $20,000 sawa na Tsh milioni 44 kwa kosa la kusambaza picha za utupu kwa watoto na udhalilishaji.
Comments
Post a Comment