Baada Ya Joti Kufunga Ndoa::Alichosema Mc Pilipili kuhusu harusi ya Mpoki....
Mc Pilipili amesema hayo katika mahojiano na Bongo5 na kueleza kuwa hata katika harusi na Joti alitamani kufanya hivyo pia.
“Mpoki nitapenda sana niwe Mc wa harusi yake na hata harusi ya Joti ilipoanza nilitamani sana kuwa Mc wa harusi yake na hata Joti mwenyewe alijitahidi sana lakini nilikuwa tayari nimeshapokea sherehe nyingine, kwa hiyo sasa hivi mtu ambaye natamani ni Mpoki” amesema Mc Pilipili.
Alipoulizwa kwa upande wake angetamani nani kufanya hivyo, alibu; “Nina marafiki wengi ma-Mc wa kawaida kama Luvanda ambaye is my very best friend to me, is like my dad, sasa sijajua awe msimamizi au kwa wazazi au awe Mc lakini pia Chris Mauki namfikiria, Samsasali pia naye namfikiria, so sijajua lakini tutakapoanza nitapenda Mc mcheshi”

Comments
Post a Comment