KASHESHE: Mwenyekiti anaedaiwa kugawa viwanja kwa Wanawake wenye makalio makubwa aongea
habari iliyosambaa sana kutoka Dodoma kuhusu Mwenyekiti wa Mtaa wa Mtakuja kata ya Chang’ombe Issa Yusuph kudaiwa kufanya upendeleo na kugawa viwanja kwa Wanawake wenye makalio makubwa.
AyoTV na millardayo.com zimempata Mwenyekiti huyo na ameanza kwa kusema >>> “Kwanza ukweli kabisa mimi sigawi viwanja bali nasimamia haki za watu ili wapate Wananchi, wanaogawa ni Manispaa na sihusiki na kugawa sababu mimi sio Mtaalamu, mimi ni Msimamizi tu”
“Unajua ukiwa kiongozi kunakua na mambo mengi yanayoweza kujitokeza kwahiyo vitu kama hivi vilivyosemwa sio vya ukweli, hii ni kama kuchafuliana sifa na mtu aliesambaza hii tuko kwenye utaratibu kumchukulia hatua kali” unaweza kumsikiliza mwenyewe kwa kubonyeza play hapa chini

Comments
Post a Comment