Je, Unatamani Kuacha Kuangalia Picha Za Ngono Na Unashindwa? Soma Hapa upate mbinu za kuacha
Kuacha kutazama picha za ngono kunahitaji nidhamu, ujasiri na imani ndani yake.
Kwani bado madhara yake huwa hayaonekani mbele ya macho ya mtumiaji.
Fuata hatua zifuatazo kujiachisha na tabia hii:
1.AMUA KUACHA LEO USISEME KESHO:
Mara kwa mara watu ambao wamebobea katika uangaliaji wa picha hizi, wanapomaliza kuangalia hujipa ahadi kwamba kesho tu nitaacha kuangalia.
Baadaye wanajikuta kesho haifiki, kwani kila siku ina kesho yake.
Ukitaka kweli kuacha amua muda uliopo sasa usipange kesho ambayo hujaifikia.
2.USIKAE KARIBU NA MAZINGIRA YA PICHA HIZO:
Ukitaka kujisaidia kuondokana na tatizo hili, hakikisha una kaa mazingira ambayo hayajatawaliwa na picha za ngono.Kama unatumia kompyuta, simu au hata iPad ambayo ndani yake umehifadhi picha hizo zifute sasa,na ikiwa unatumuia DVD au CD ziharibu usikae nazo ndani, na hata katika historia ya anwani ya mitandao uliyotembelea, kama zipo zifute kabisa kwani ukiziona utarudi kule kule.
3.USIHESABU SIKU AMBAZO HUJAANGALIA:
Mara nyingi kama umebobea kuangalia huwa haipiti siku bila kutupia jicho picha hizo.Na kuna muda mwingine unabanwa na shughuli nyingi kukupelekea kufikisha siku kadhaa hujaangalia,sasa usikae chini kuanza kuhesabu siku ambazo hujaangalia utajikuta unajipa kibali cha kutaka kuziangalia haraka iwezekanavyo.
4.USIKAE MAZINGIRA YA PEKE YAKO:
Mara nyingi kama uliwahi kuangalia picha za ngono na ukajikuta uko mazingira ya peke yako, ya ama unaangalia tamthilia au kusoma kitabu chochote kitakachokuwa na habari ya masuala ya watu kujamiana itakukumbusha kamchezo kako.
Usichague pia kuangalia peke yako picha ziliwekwa alama ya miaka 18 zitakuchochea urudi ulipotoka.
5.EPUKA MAZUNGUMZO MACHAFU NA MARAFIKI:
Mara nyingi tunapokaa na marafiki zako ambao wanapenda kuhadithia masuala ya ngono tu watakuchochea.Maana kuna wengine ni mafundi wa kuhadithia hizo vitu, kana kwamba wao ndiyo watengenezaji,sasa unapoona wanaanzisha hizo habari kama huwezi kuwasimamisha basi ni heri ujitenge nao.
6.EPUKA HISIA CHOCHEZI ZA NDANI:
Siri kubwa katika hizi picha zinampa hisia nzuri mtazamaji, na kuona hakuna chenye thamani yoyote muda huo.Kwa hiyo epuka hisia za hasira, upweke, na huzuni kwani zitakufanya uone eneo pekee la kwenda kujipumzisha ni kuangalia picha hizo.
7.FUTA FIKRA POTOFU:
Achana na fikra potofu za mtaani kuwa kuangalia picha za ngono ni kujifurahisha nafsi na hazina madhara.Lakini kiuhalisia madhara yanayoambatana na tukio lake utayaona baadaye.Kuna wengine watakwambia kuwa usipoangalia hizo picha utakuwa mshamba na hauendi na wakati.
8.USIJISEMESHE KUWA HUWEZI KUACHA:
Unapokuwa unaangalia hizi picha mara nyingi akili yako inajizoesha, na kuona ni utaratibu wake wa kila siku.Kwa hiyo moyoni utakuwa unajisemesha kuwa kuacha kitendo hiki hautaweza kamwe,kitu ambacho kitakufanya uwe dhaifu wa kujitawala.
9.ACHA KUJIKUMBUSHA PICHA ULIZOANGALIA:
Mara nyingi unapokuwa mazingira fulani ya kuwaza mambo mbali mbali, mawazo ya picha ulizoangalia ukiyatanguliza kwanza utajifanya uwe na shauku ya kwenda kuangalia upya.ukiona kuna kazi unafanya kazi katika kompyuta au umeshika kifaa chochote chenye uwezo wa kukuonesha picha hizo ni heri ukizime kwa muda huo halafu fikiria kitu kingine kwa haraka.
Comments
Post a Comment