Hawa Ndio Wakuu Wa Mikoa Wapya Na Waliotumbuliwa


Balozi Kijazi amesema katika nafasi za wakuu wa mikoa, Rais Magufuli amewateua wa mikoa sita, miongoni mwao ni aliyewahi kuwa waziri katika utawala uliopita wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Adam Malima anayekwenda Mkoa wa Mara.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti amepandishwa cheo na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Balozi Kijazi amesema wakuu wa mikoa walioondolewa kutokana na kustaafu ni Joel Bendera (Manyara), Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga (Geita) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi mstaafu wa Polisi, Zelothe Stephen (Rukwa).

Wakuu wa mikoa walioachwa ni wa Mtwara, Halima Dendego, Jordan Rugimbana (Dodoma) na Dk Charles Mlingwa (Mara).

Amesema Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Joackim Wagambo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Robert Gabriel amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christine Mndeme akiwa mkuu wa mkoa huo.

Galesius Byakanwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Comments

Popular posts from this blog

Kweli Dunia Imeisha::: Unaambiwa Hizi Ndio Bei Za Makahaba/Machangudoa Dar......Sinza Hakushikiki

Hizi Ndizo Shida Tatu Kubwa Za Mwanamke Mwenye Makalio Makubwa Awapo Kwenye Kitanda Soma Hapa

Kitakachompata Mwanamke Endapo Akiacha Kufanya Mapenzi Soma Hapa