Diamond Awa Msanii Wa Kwanza Afrika Kupata Tuzo Hii Kubwa Duniani...Team Kiba Watowa Povu
Msanii wa Bongo Flava, Diamond Platnumz amepatiwa tuzo na label ya Universal Music Group (UMG) hapo jana October 27 mara baada ya wimbo wake Marry You aliomshirikisha Ne-Yo kufikisha mauzo ya platinums sita, hivyo kumfanya kuwa msanii wa kwanza Afrika chini ya label hiyo kufikisha idadi hiyo ya mauzo.
Leo nimekuwa msanii wa kwanza wa kiafrika alosainiwa Universal Music Group kufikisha Mauzo ya nyimbo yake Platinum Mara sita Mfululizo kupitia nyimbo ya #MarryYou nilomshirikisha @Neyo…. kwa niaba ya Team yangu na @neyo tungependa kuwashukuru Mashabiki na Media zote Ulimwenguni…) #ABoyFromTandale
Ujumbe huo aliandika Diamond katika mtandao wa kijamii wa Instagram akielezea furaha yake ya kushinda tuzo hiyo, hata hivyo Baby Mama wake, Zari The Boss Lady naye alimchukua muda wake na kumpongea Diamond kwa kuandika;.
Congrats babe @diamondplatnumz for becoming the first African Artist signed under Universal to hit Six times platinum sales on your #MarryYouft @Neyo Record! Am super Proud!
Comments
Post a Comment