Breaking News::: Taarifa Mpya Kuhusu Afya Ya Tundu Lissu Soma Hapa
DONDOO JUU YA TAARIFA YA MHE.LISSU ILIYOTOLEWA LEO NA MHE.FREEMAN MBOWE.
1. Wiki iliyopita kwa mara ya kwanza Mhe.Lissu alitoka ICU.
2. Tayari mashine za kuimarisha figo alizokuwa akitumia zimeondolewa.
3. Kwa sasa hatumii tena mirija wakati wa chakula. Anakula kawaida na chakula anachokitaka.
4. Hatumii tena hewa maalum ya Oksijeni.
5. Juzi kwa mara kwanza AMEKAA na kwa sasa anatembea kwa wheelchair.
6. Jopo la madaktari 12 limehusika katika matibabu yake.
7. Baada ya wiki moja, Mhe.Lissu atamaliza awamu ya pili ya matibabu na baada ya hapo ataanza matibabu ya awamu ya tatu nje ya Kenya na nje ya Tanzania (Kwa sasa nchi anayopelekwa Mhe.Lissu haitawekwa wazi kwa sababu za kiusalama mpaka hapo baadae).
8. Katika awamu hii ya tatu ya matibabu (rehabilitation), familia ya Lissu itapokea zamu ya kuhusika zaidi naj kuwa wasemaji kwa kuwa sasa Mhe.Lissu ameshajitambua kwa ufahamu wake. Sisi kama chama tutabaki kutoa support kama tulivyoanza.
9. Picha za Mhe.Lissu zitaanza kutoka rasmi kuanzia leo. Pia muda mfupi ujao, mtaanza kumikia Mhe.Lissu kwa sauti yake na mtaziona videos zake.

Comments
Post a Comment